The House of Favourite Newspapers

WATOTO WA MASTAA WANAOTIKISA MITANDAONI – VIDEO

Latifah Nasibu ‘ Princess Tiffah ‘

MITANDAO ya kijamii kama Instagram, Facebook, Twitter, YouTube, Vimeo, Snapchat na mingineyo mingi, hivi sasa ni biashara kubwa mno duniani.

 

Biashara hii inatajwa kukua kwa kasi ya ajabu kutokana na maendeleo ya teknolojia ya habari.Biashara hii inafanywaje? Ishu ni kuwa na ufuasi wa watu wengi kisha kifuatacho ni matangazo yatakayokuwa yakilipiwa na kuingiza mkwanja kama wotee.

 

Umuhimu wa mitandao ya kijamii hasa Instagram kwa ukanda wetu umeongezeka mno. Mastaa wa muziki na filamu za Kibongo wamekuwa wakishindana kuwa na wafuasi (followers) wengi kwenye Instagram na kujitangaza kazi zao za sanaa.

 

Ukiacha mastaa wakubwa, vita ya followers pia imehamia kwa watoto wa mastaa hao ambao sasa wanatikisa kwa kuwa na followers kibao mitandaoni kisha kujikuta wakipata matangazo ambayo yanawaigizia mkwanja unaowasaidia wazazi wao kuwalea na kuendeshea maisha.

 

Hata hivyo, uchunguzi wa Gazeti la Amani ulibaini kwamba akaunti za watoto hao zinaendeshwa na wazazi wao kwani sheria za Instagram haziruhusu mtoto chini ya umri wa miaka 13 kuwa na akaunti kwenye mtandao huo.

1: PRIN-CESS TIFFAH

Latifah Nasibu almaarufu Princess Tiffah ni mtoto wa kike wa staa grade one wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aliyezaa na mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Princess Tiffah almaarufu Tiffah Dangote ndiye mtoto maarufu zaidi kwa sasa Afrika Mashariki. Tiffah aliyezaliwa Agosti 6, 2015, ana jumla ya Followers milioni mbili.

2: PRINCE NILLAN

Nillan Nasibu ‘Princes Nillan’ ni mtoto wa pili wa Diamond na wa tano kwa Zari. Mtoto huyu wa kiume anashika nafasi ya pili kwa kuwa na followers wengi kwenye Instagram.

Nillan ana jumla ya followers 749,000.

3: COOKIE

Cookie Moses ni mtoto wa kike wa mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel aliyezaa na dansa wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo. Akaunti ya Cookie ya Instagram ina jumla ya followers 484,000.

4: DYLLAN

Dyllan Nasibu au Young Lion ni mtoto mwingine wa kiume wa Diamond aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto. Dyllan anashika nafasi ya nne kwa kuwa na followers wengi kwenye Instagram ambao 398,000. 

5: JAYDAN

Namba tano inakwenda kwa mtoto wa msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ aliyezaa na video queen Fahyma. Akaunti ya mtoto huyo kwenye Instagram ina followers wapatao 214,000.

6: JADEN

Mtoto wa staa wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ aliyezaa na mwigizaji mwenzake, Chuchu Hans, Jaden Vincent anashika nafasi ya sita kwa kuwa na followers wengi.

Jaden anayezua gumzo kutokana na uzuri wake, ana jumla ya wafuasi 183,000.

7: KIBA JUNIOR

Kiba Junior ni mmoja wa watoto wa staa mwingine wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’. Ndugu zake wengine ni Sameer Ali na Amaya Ali.

Akaunti ya Kiba Junior kwenye Instagram ina followers 134,000.

8: SASHA DESIDERIA

Sasha ni mtoto wa mwanamuziki ambaye ni Mbunge wa Mbeya-Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliyezaa na mwanamama wa filamu za Kibongo, Faiza Ally.

Kwenye akaunti yake ya Instagram ana followers 122,000.

9: PRINCES TANZANITE

Huyu ni mtoto wa kike wa msanii wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhani ‘H Baba’ na mwigizaji wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi. Tanzanite ana jumla ya wafuasi 75,800.

10: FANTASY

Fantasy ndiye anayefunga listi hii. Ni mtoto wa mmiliki wa Radio EFM na mwanamitindo Hamisa Mobeto. Fantasy ana followers 74, 800.

NA SIFAEL PAUL | GLOBAL PUBLISHERS

====TOP 10 ya Watoto wa mastaa wanaotikisa Instagram Bongo===

Comments are closed.