The House of Favourite Newspapers

Watoto wa Mzee Yusuf: Yupo Wapi Mama?

0
Mzee Yufuf na watoto wake (Picha hii ni kwa hisasi ya Salute 5)

HAKIKA ni huzuni! Zikiwa zimepita siku kumi tangu apate pigo la kufiwa na mkewe mdogo, Chiku Khamis, aliyekuwa Mfalme wa Taarab Bongo na Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern, Alhaj Mzee Yusuf kwa mara ya kwanza ameibuka na kueleza jinsi watoto wake wanavyomlilia mama yao.

 

Akizungumza na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Mzee Yusuf alisema mara baada ya mkewe kufariki, watoto hao walikuwa wakilia sana huku wakiuliza alipo mama yao.

 

AWAPELEKA KWA NDUGU WA MAMA YAO

Mfalme huyo aliyeacha ghafla muziki na kumrejea Mola wake, alisema kutokana na kilio cha watoto wake, alilazimika kuwaruhusu ndugu wa mama yao, wawachukue, japo kwa muda ili kupunguza machungu yao.

 

“Ninapata taarifa kuwa watoto hawaishi kuuliza alipo mama yao na kila wakikumbuka wanalia, hili ni jaribio kubwa ambalo atalazimika kupigana ili kuhakikisha linaisha salama.

Mzee Yusuf na aliyekuwa mkewe, Chiku Hamis enzi za uhai wake.

 

ATAKA KUKAA NAO MWENYEWE

“Nadhani huu muda ambao wamekaa kwa ndugu wa mama zao hao unatosha, hivyo nakwenda kuwachukua ili nikae nao mwenyewe, nianze nao maisha mapya ya bila mama yao kwa sababu nahisi ndiyo faraja yangu kwa sasa.

 

“Sijawa na maisha, bado nimechanganyikiwa, hivyo naamini nikienda kuwachukua watakuwa faraja yangu maana nikiwa nao naona niko salama zaidi, watoto wangu nitakaa nao mwenyewe maana mimi ndiye baba yao, watakaa na nani tena kama siyo mimi?

Jeneza lilobeba mwili wa marehemu Chiku Hamis

 

“Naanza kazi na maisha upya na watoto bila mama yao, kikubwa naomba mashabiki waniombee ili niushinde mtihani huu nilioupata, nitawalea mwenyewe maana mama yao ndiyo hivyo ameondoka, hivyo siyo kwamba watakaa na mke mkubwa, watakaa na mimi,” alisema Mzee Yusuf.

 

Kifo cha Mke wa Mzee Yusuf… Simanzi, Majonzi, Vilio na Huzuni!

Leave A Reply