The House of Favourite Newspapers

Watu 11 Wauawa Katika Shambulio Brazil

TAKRIBAN watu 11 wameuawa baada ya watu wenye silaha kuvamia baa moja na kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwemo ndani ya baa hiyo iliyopo katika jimbo la Para kaskazini mwa Brazil.

 

Msemaji wa jimbo hilo, Natalia Mello, amesema washambuliaji hao waliokuja wakiwa kwenye magari na pikipiki waliwashambulia watu hao kabla ya kukimbia.

Mello amesema vifo hivyo vilihusisha wanawake sita na wanaume watano ambapo  polisi wamesema washambuliaji hao walikuwa saba, na mmoja alijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Comments are closed.