The House of Favourite Newspapers

Watu 123 Wafariki Dunia Baada Ya Lori Kulipuka

0

Watu 123 wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka katika mji wa Ahmedpur Sharqia, Punjap nchini Pakistan.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyogharimu maisha ya watu 123 huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Imeelezwa kuwa baadhi yao walipoteza maisha wakiwa wanajaribu kuteka mafuta kutoka kwenye lori hilo mara baada ya kupinduka. Majeruhi wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali mara baada ya gari hilo kupinduka walikuwa wakivuta sigara, jambo ambalo limeelezwa kuwa chanzo cha moto huo.

Chanzo BBC.

Leave A Reply