The House of Favourite Newspapers

Watu 29 Wajeruhiwa Kwenye Mlipuko New York, Marekani

shambulioJose Vasquez mmoja wa majeruhi wa shambulio hilo.  shambulio-chelsea-new-2Kikosi cha uokoaji kikiwa kimembeba mmoja wa majeruhi.shambulio-chelsea-new-4Eneo la tukio.shambulio-chelsea-new-5Baadhi ya vitu vilivyoharibiwa kwenye mlipuko huo.

shambulio-chelsea-new-1Meya wa Jiji la New York, Bill de Blasio  akizungumza baada ya shambulio hilo.

Mlipuko umetokea jijini New York, katika eneo la Chelsea, Wilaya ya Manhatan ambapo watu 29 wamejeruhiwa. Katika mlipuko huo hakuna aliyefariki.

Polisi wanashuku huenda mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kilipuzi na wanaendelea na uchunguzi kubaini ukweli wa mambo.

Meya wa New York, Bill de Blasio amesema mlipuko huo ulisababishwa kwa makusudi lakini akasisitiza kuwa hadi sasa haujahusishwa na kundi lolote la kigaidi.

Amesema pia kuwa hakuna ushahidi kuwa mlipuko huo una uhusiano wowote na bomu la mfereji lililolipuka katika jimbo jirani la New Jersy saa chache zilizopika.

Bomu hilo lililipuka karibu na mahali ambapo mbio za kukusanya pesa za kuwasaidia wanajeshi wa zamani zilikuwa zikiendeshwa.

 

Comments are closed.