The House of Favourite Newspapers

Watu 70 Wafariki Katika Mapigano Yemen

0

WATU 70 wameuwawa baada ya kutokea mapigano makali kwenye maeneo matatu tofauti katika kipindi cha masaa 24 huko katika mji wa Marib nchini Yemen.

 

Wapiganaji tiifu kwa serikali ya Yemen wanasema vifo hivyo vinawahusisha wapiganaji wa upande wa serikali pamoja na wa kundi la waasi wa Huthi.

 

Wakinukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP maafisa wawili wa kikosi kinachoegemea upande wa serikali wamesema makabiliano hayo yamesababisha wapiganaji wao 26 kupoteza maisha huku waasi wakiwa 44, Ingawa kwa upande wa uasi imekuwa vigumu waasi kueleza athari wanazozipata.

 

Tangu mwezi Februari, kundi la Huthi limekuwa katika jitihada za kuudhibiti mji wa Marib, ambao ni mji mkuu wa mkoa wenye hazina kubwa ya mafuta na eneo muhimu kwa kujikusanyia mapato kwa serikali ya Yemen kwa upande wa kaskazini.

 

Mgogoro wa Yemen umesabababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na kuwasabisha wengine mamilioni kukumbwa na balaa la njaa, katika kile Umoja wa Mataifa unakiita “Janga baya zaidi la kiutu duniani.”

 

Leave A Reply