The House of Favourite Newspapers

Watu Saba Wafariki Uingereza Baada ya Kuchanjwa Covid 19

0

WATU saba wamefariki nchini Uingereza kutokana na damu kuganda mwilini baada ya kupewa chanjo ya Oxford-AstraZeneca, mamlaka ya kudhibiti dawa imethibitishia BBC.

 

Kwa ujumla watu 30 kati ya milioni 18 waliopewa chanjo hiyo kufikia Machi 24 wamekabiliwa na hali ya damu kuganda.

 

Bado haijulikani ikiwa ni bahati mbaya tu au athari ya kweli ya chanjo.

 

Shirika la udhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya linanasema faida ya chanjo zinaendelea kuzidi madhara yake.

 

Hata hivyo, hali ya kuganda kwa damu kwenye ubongo, kitaalamu “cerebral venous sinus thrombosis” au CVSTs zimesababisha nchi nyingine – zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Canada – kudhibiti utumizi wa chanjo hiyo.

 

Shirika la Afya duniani na Wakala wa Dawa wa Ulaya wanasema faida za chanjo hiyo zina faida Zaidi kuliko ,madhara

Leave A Reply