The House of Favourite Newspapers

Watu Wasiojulikana Wafukua Kaburi Usiku na Kuikata Maiti Sehemu za Siri Kisha Kuifukia

0

Watu wasiojulikana wamefukua kaburi na kuondoa sehemu za siri za mwili wa marehemu Ruben Kasala (74) uliozikwa majira ya saa 11:30 jioni mnamo Machi 18, 2023 katika Kijiji cha Kasokola Kata ya Kasokola Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Akizungumza mtoto wa marehemu Kasala, Frank Kasala amesema baba yao alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari na pia alikuwa na shida kwenye mapafu lakini ilipofika siku ya tarehe 18 asubuhi, walipokea taarifa ya msiba na siku hiyohiyo wakafanya shughuli za maziko.

Amesema, kutokana na mila na desituri zao iliwalazimu asubuhi yake kurudi sehemu walipomzika baba yao na baada ya kufika walikuta kaburi limefukuliwa na sanduku kuvunjwa ambapo baadae walizika upya huku wakiwa hawajui sababu iliyopelekea mwili huo kufukuliwa na kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasokola Carlos Joakim amesema alipokea taarifa ya kifo majira ya saa 1:30 asubuhi na walikubaliana kuzika siku hiyohiyo lakini siku inayofuata alipata taarifa ya kuwa kaburi hilo limefukuliwa na kuamua kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi.

Akizungumizia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ACP Alli Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

“Tulipofunua ile coffin (Jeneza) ikabainika kwamba sehemu za siri za huyo marehemu zilikuwa zimeondolewa, na baadae kurudisha mfuniko ule wa coffin, wakarudishia na udongo”

Kamanda Makame amewaasa wananchi wa mkoani humo kuachana na imani potofu za kufikia hatua ya kufukua miili ya marehemu ambayo tayari imeshasitiriwa.

Leave A Reply