The House of Favourite Newspapers

BREAKING NEWS: WATANO WAFARIKI AJALINI MANYONI, SINGIDA

WATU watano wamefariki jioni ya leo baada ya gari dogo linalomilikiwa na Wizara ya Kilimo na Chakula kupinduka katika eneo la Njiri wilayani Manyoni mkoani Singida.

Kamanda ya Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike, amethibitisha kwamba ajali hiyo imehusisha magari mawili, moja lenye namba za usajili STK  8925 la Wizara ya Kilimo na Chakula  ambalo lilikuwa linatoka Dodoma kwenda Shinyanga, na lori  (semi-trailer) lililokuwa linaelekea Dar es Salaam lenye usajili wa RIC 152Y ambayo yaligongana uso kwa uso.

“Watu watano waliokuwa kwenye gari dogo wote wamefariki huku dereva na utingo waliokuwa kwenye lori wakiwa wamejeruhiwa,” alisme kamanda huyo na kuongeza kwamba chanzo cha ajali hiyo kilitokana na uzembe wa gari dogo aliyetaka kuyapita magari mengine bila kuwa na tahadhari,” alisema ACP Njewike.

Comments are closed.