The House of Favourite Newspapers

Watu Watatu Watiwa Mbaroni kwa Kuiba Ng’ombe wa Rais Museveni

musevenRais Museveni

KAMPALA: Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Kampala, Uganda kwa tuhuma za kuiba ng’ombe ambao idadi yake haijajulikana vizuri katika shamba la Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni, polisi walisema jana Jumapili.

“Mmoja kati yao anafanya kazi kwenye shamba la rais Museveni. Walikuwa wakipeleka ng’ombe hao mnadani kuuza,” Mkuu wa Kituo cha Polisi, Doreen Kachwo aliiambia AFP.

ngombe“Watuhumiwa hao wamekiri kuiba ng’ombe hao na wamekuwa wakifanya hivyo mara kadhaa hata kabla ya kukamatwa,” aliongeza.

“Baada ya uelelezi kukamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma za wizi zinazowakabili.”

Shamba kubwa la rais Museveni la Kisozi  lipo wilayani Gomba, katikati mwa Uganda, ambapo ni takribani kilomita 100 Magharibi mwa Kampala, ambapo kabila la Banyankore linapatikana.

museveniaMuseveni akiwa na mkewe, Janeth Museveni.

Museveni hupendelea kwenda kule kupumzika hata wakati mwingine kupeleka wageni wake wanaokwenda kumtembelea kutoka nje ya nchi hiyo.

Museveni, ameiongoza Uganda kama rais wa nchi hiyo kwa miongo mitatu sasa tangu mwaka 1985 ambapo mwezi Febuari mwaka huu, Museveni alichaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo baada ya kumshinda mpinzani wake, Kizza Besigye aliyepinga matokeo ya uchaguzi huo.

Comments are closed.