The House of Favourite Newspapers

Watu wenye silaha wavamia hoteli na kuteka watu Mali

0

1

Wanajeshi wakijaribu kuingia katika Hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako.

3Hoteli ya Radisson Blu iliyovamiwa leo.

Wanajeshi wenye silaha nchini Mali wameingia katika hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako baada ya watu wenye silaha kuishambulia na kuwashikilia watu mateka.

Uvamizi huo ulitekelezwa leo asubuhi kwenye hoteli hiyo ya kifahari ambayo hupendwa sana na watu wa mataifa ya nje.

2

Baadhi ya wananchi wakiokolewa kutoka kwenye hoteli ya Radisson Blu.

Ripoti zinasema mateka 80 wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ambayo inamilikiwa na Wamarekani.
Awali, kampuni inayomiliki hoteli hiyo ya Rezidor Hotel Group ilisema watu 170 walikuwa wameshikiliwa mateka na watu hao.

Baadhi ya ripoti zinasema watu walioshambulia hoteli hiyo yenye vyumba 190 huenda wakafika 10.

Leave A Reply