The House of Favourite Newspapers

Watuhumiwa Mauaji ya Bondia Mashali Warudishwa Rumande

mashaliNa Gabriel Ng’osha, Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Toleo la Desemba 21, 2016

DAR ES SALAAM: Vijana saba wanaoshtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Bondia Thomas Mashali, jana walirudishwa rumande kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam inayosikiliza kesi hiyo namba IP 29, chini ya Hakimu Boniface Lyamike na mwendesha mashtaka Monica Ndakidema.

Watuhumiwa hao ni Issa Kasim Swadaka, Ramadhani Ally, Athuman Bakari, Charles Fadhili Manongi, Mohammed Kassim Kyamba, Joseph Yacob Maro na Emmanuel Michael Paschal, ambao awali walifikishwa mahakamani hapo Desemba 8, mwaka huu na kusomewa mashitaka yao huku wakinyimwa dhamana kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi yao.

Kesi hiyo itafikishwa tena mahakamani hapo Januari 3, mwakani kwa ajili ya kutajwa. Marehemu Thomas Mashali  aliuawa Oktoba 30 na kuzikwa Novemba 2, mwaka huu baada ya kupigwa na watu wasiojulikana maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Mwanafunzi wa Chuo cha Bandari, Thomas Lucas Magula (21), mkazi wa Kigamboni anayedaiwa kujifanya Shilole, anayekabiliwa na kesi ya kutukana watu kwenye mtandao wa kijamii kupitia jina la Shilolekiunooficial, ameachiwa huru kwa dhamana ambapo kesi yake itasikilizwa tena Januari 16, mwaka 2017.

Darassa Anusurika Kifo kwa Ajali Hii Mbaya ya Gari Huko Kahama Shinyaga

Comments are closed.