The House of Favourite Newspapers

Haya Ndio Maisha Halisi ya Ben Pol, Mbali na Muziki Sana Analima Vitunguu

ben-pol-6   Mwanamuziki mahiri wa Bongo Flava, Bernard Paul ‘Ben Pol’  akiwa na mtoto wake nyumbani kwake Tabata- Aroma, jijini Dar.

MAKALA YA MPAKA HOME: Na Imelda Mtema | Gaztei la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 17, 2016

MAMBO vipi mtu wangu wa nguvu, mimi hapa kazi yangu ni moja tu kukufanya wewe msomaji wangu kufurahia kile unachokiona na kukisoma ndiyo maana kila wiki najitahidi kukuletea makala haya ya Mpaka Home, yakiwahusu watu maarufu uwapendao.

ben-pol-1Muandishi wa makala hii ya Mpaka Home, Imelda Mtema akiwa nyumbani kwa Ben Pol.

Wiki hii mguu wa safu hii ulitia nanga Tabata- Aroma, jijini Dar, nyumbani kwa mwanamuziki mahiri wa Bongo Flava, Bernard Paul ‘Ben Pol’ ambaye leo hii utayajua maisha yake halisi nje ya muziki.
Nyumbani hapo anaishi na mama mtoto wake aitwaye Ratifa pamoja na mtoto wake wa kiume aliyempa jina la Mali.
Kwa nini nikumalizie uhondo huku juu? Mimi na wewe twende pamoja hapa chini uweze kujua mengi zaidi.
Mpaka Home: Kaka mzima, sijajua kama una mtoto, umempata lini?

ben-pol-3Wakipata chochote kabla ya mahojiano.

Ben Pol: Haaa huyu mbona kitambo maana sasa hivi ana umri wa miezi nane.
Mpaka Home: Mama yake yuko wapi maana nakuona uko bize kumbem-beleza peke yako?
Ben P0l: Kaenda kwenye shughuli zake za kila siku hata mimi kuwepo hapa ni kwa sababu nilikuwa nasubiri kuonana na wewe.
ben-pol-5Mpaka Home: Naona unaishi na mama Mali je, mmeshafunga ndoa?
Ben P0l: Bado, ila Mungu akipenda tutafunga hapo baadaye, kwa sasa tunajipanga kwanza.
Mpaka Home: Japokuwa wewe ni staa lakini nakuona unamfanyia kila kitu mwanao tofauti na akina baba wengine, hii ikoje?
Ben Pol: Linapokuja suala la malezi ya mwanangu, ustaa nauweka pembeni.

ben-pol-4Ben Pol akifanya mazoezi.

Mpaka Home: Maisha yako ya kila siku hapa nyumbani yapoje?
Ben Pol: Ni ya kawaida sana yaani kama yalivyo ya watu wengine, hakuna tofauti kama vitumbua nakula, mihogo nakula, ugali ndiyo usiseme. Maisha ni yaleyale tu.
Mpaka Home: Unakumbuka ni lini mara ya mwisho kupanda daladala?
Ben Pol: Ni muda mrefu sana sijapanda daladala.

img_4424Ben Pol akiwa na mtoto wake.

Mpaka Home: Ni kwa sababu gani au kitu gani unahofia wakati ndiyo usafiri wetu wa kila siku?
Ben Pol: Unajua kuna wakati natamani kutumia usafiri huo, lakini kwetu sisi mastaa inakuwa shida maana kwenye hilo gari itakuwa ni usumbufu ndiyo maana sipendi kupanda daladala.
Mpaka Home: Maisha ya umaarufu na kabla hujawa maarufu kuna tofauti yoyote?
Ben Pol: Tofauti ni kubwa sana, unapokuwa siyo maarufu kitu chochote unaweza kufanya maana mimi leo siwezi hata kutoka nje ya geti langu kupunga upepo, watajazana watu, sasa hiyo inakuwa shida kwa sababu kuna wakati unatamani kuishi maisha ya kawaida.

ben-pol-7
Mpaka Home: Unafikiri kuna kitu kimebadilisha maisha yako?
Ben Pol: Ndiyo! Kupata mtoto ni kitu kikubwa sana kwani amebadilisha maisha yangu.
Mpaka Home: Mastaa wengi wana tabia ya kukataa watoto wanapowazaa vipi wewe umeweza kukubali kirahisi na kuonyesha mapenzi kwa mwanao?

img_4479
Ben Pol: Siwezi kuikataa damu yangu kwa kuwa najua mimi ndiyo muhusika, nafsi itanisuta na sitaweza kufanikiwa maishani.
Mpaka Home: Kuna baadhi ya watu wanasema wewe unaringa vipi kuhusu majirani zako unaoishi nao?
Ben Pol: Unajua mtu ambaye hajawahi kukaa na wewe hawezi kukujua vyema maana akisema unaringa ni kwa sababu huwezi kukutana na kila mtu njiani ukasimama kwani unaweza usifike hata unakokwenda lakini mimi nipo poa hata kwa majirani zangu.
Mpaka Home: Nje na kazi ya muziki kuna kitu kingine unachofanya?
Ben Pol: Ukiacha muziki, mimi ni mkulima mzuri tu wa vitunguu, ninalima Moshi na Mbeya kitu ambacho kinanifanya maisha yanasonga zaidi.
Mpaka Home: Hapo nje nimekuta vifaa vya mazoezi na wewe ni mdau wa kuweka mwili fiti?
Ben Pol: Sana tu ni lazima nifanye hivyo asubuhi na mapema kwani mazoezi yananifanya niwe na afya njema.
Mpaka Home: Unapopata muda wa kuwa nyumbani unapenda kufanya nini?

ben-pol-9Akiangalia vitunguu vyake.

Ben Pol: Napenda kuangalia runinga hasa muziki na kucheza na mtoto wangu.
Mpaka Home: Hapa unapoishi ni nyumba yako au umepanga?
Ben Pol: Hapa nimepanga lakini Mungu akijalia siku si nyingi nitakuwa kwangu.
Mpaka Home: Katika wimbo wako wa kwanza uitwao ‘Nikikupata’ ulimuimbia Latifa mama wa mtoto wako au ni utunzi tu?
Ben Pol: Hapana, nikiwa kidato cha sita nilitokea kumpenda msichana mmoja nikamtungia wimbo huo lakini hadi leo sidhani kama anajua ndiye niliyemuimba.
Mpaka Home: Nakushukuru sana Ben Pol kwa ushirikiano wako.
Ben Pol: Karibu.

ben-pol-10

Muonekano wa nje wa nyumba anayoishi Ben Pol.

Haya ndo maisha halisi ya Ben Pol

Comments are closed.