Watuhumiwa wa Mauaji ya Watoto Njombe Wafikishwa Kortini

WATUHUMIWA watatu wa matukio ya mauaji ya watoto mkoani Njombe, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe akiwemo Joel Nziku ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja ya Danford Nziku mkazi wa Ikando, Njombe, leo Jumanne February 12, 2019.

Watuhumiwa wengine ni Nasson Kaduma na Alphonce Danda. Nje ya mahakama hiyo ulinzi umeimarishwa huku askari wa Jeshi la Polisi wakitapakaa kila kona na msafara wa watuhumiwa hao ukisindikizwa na magari sita ya polisi.

Loading...

Toa comment