The House of Favourite Newspapers

Kiongozi wa Serikali Anusurika Kifo Baada ya Paa la Kanisa Kuanguka, Waumini 200 Wapoteza Maisha

kanisaa-1

UYO, NIGERIA: WATU zaidi 200 wamepoteza maisha huku wengine ambao idadi yao haijkafahamika wakijeruhiwa baada ya paa la kanisa walimokuwa wakisali kuwaangukia wakati wa ibada jana Jumamosi, Desemba 10, 2016 katika Mji wa Uyo, nchini Nigeria.

kanisaa-2Kanisa hilo la Reigners Bible Ministry lililopo mjini Uyo, Akwa Ibom, japokuwa bado halijakamilika kujengwa lakini waumini wamekuwa wakilitumia kwa ajili ya ibada na jana Jumamosi inasemekana lilikuwa limefurika waumini wakati paa linaanguka na kusababisha madhara hayo.

kanisaa-3Miili ya watu 60 iliokotwa katika eneo la tukio huku waumini wengine wengi wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ambako mauti yamewakuta ambapo mpaka sasa ni zaidi ya waumini 200 ambao wameripotiwa kupoteza maisha na inasemekana huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Gavana wa Mji wa Akwa Ibom, Bwana Udom Emmanuel aliyekuwemo kanisani humo wakati wa ibadaba amenusurika kifo baada ya kujiookoa wakati wa maafa hayo. Imeelezwa kuwa Gavana Udom alitoka salama bila kujeruhiwa.

Msemaji wa gavana huyo, Ekerete Udoh, amesema kuwa kuna haja ya mamlaka ya serikali kuunda chombo kitakachochunguza ubora wa jengo hilo au kama endapo kuna mtu alifanya jambo fulanikwa niaba ya kuliporomosha kanisa hilo.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ameelezea majonzi yake kutokana na vifo hivyo na kutuma salam za rambirambi kwa ndugu wa marehemu hao ambapo pia ametoa salam za pole kwa majeruhi waliotokana na tukio hilo.

Mnamo Septemba 2014, watu115 wakiwemo WaafrikaKusini 84, walipoteza maisha nchini Nigeria baada ya Kanisa la Mhubiri maarufu Afrika, Nabii Joshua (T B Joshua) kuanguka jijini Lagos.

 CREDIT: punchng.com & aljazeera
halotel-strip-1-1

Comments are closed.