The House of Favourite Newspapers

Nape Nnauye: Tuzo Za EATV Zitafanya Rais Magufuli Aendelee Kuniacha

eatv-14Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto)  akimsikiliza Bonny Love mshindi wa tuzo ya heshima.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika usiku kuamkia leo Mlimani City alifunguka na kusema kazi waliofanya EATV na tuzo za EATV AWARDS anaamini kuwa hata Rais Magufuli ataendelea kumuacha acha kidogo katika wizara hiyo.

napeWaziri Nape alisema hayo wakati akimkabidhi Dj Bonny Love tuzo ya heshima na kusema kazi kubwa iliyofanywa na waandaaji wa tuzo hizo itamfanya mpaka Rais Magufuli aendelee kumuacha acha kidogo kwani anaonekana na yeye akifanya kazi vyema.

“Kwanza napenda kuwapongeza waandaaji wa tuzo hizi kiukweli mmefanya kazi nzuri sana, kwa kazi nzuri hii lazima Mhe. Rais Magufuli ataendelea kuniacha acha kidogo kwani anaona nikifanya kazi” alisema Waziri Nape Nnauye

Mbali na hilo Waziri Nape Nnauye aliwataka watanzania kuwa wavumilivu na kusema wataacha kubana kama ambavyo amekuwa akiaambia mtaani kuwa wamebana sana hivyo milango itafunguliwa na mambo kuwa sawa mtaani.

“Tutaachia kidogo hatutabana sana, na mimi nimepita mtaani nimeambiwa Nape mmebana sana. Wakati wmingine tunataka kufanya mambo tunaambiwa tumepitiliza ila wakati mwingine tutafunga jicho moja watu wapitilize ili mambo yaende sawa sawa”. Waziri Nape Nnauye

Comments are closed.