The House of Favourite Newspapers

Wawili Wafariki Kwenye Maandamano Myanmar

0

IDARA ya huduma za dharura nchini Myanmar imesema, watu wawili waliuawa katika mji wa Mandalay jana Jumamosi Feb. 20 wakati walinda usalama walipofyatua risasi ili kuwatawanya waandamanaji wanaopinga mapinduzi ya kijeshi ya Februari mosi.

Waandamanaji walikusanyika katika miji mikubwa na midogo kote nchini Myanmar wakiwemo jamii za makabila madogo, watunzi wa mashairi, wasanii na wafanyakazi wa sekta ya uchukuzi, kudai utawala wa kijeshi uondoke madarakani na kuachiliwa kiongozi aliyechaguliwa Aung San Suu Kyi na wanasiasa wengine waliopo kizuizini.

 

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amelaani hatua zilizochukuliwa na vikosi vya usalama nchini Myanmar na amevitaka kuacha mara moja kuwabughudhi raia.

Leave A Reply