The House of Favourite Newspapers

JPM Awataka Watanzania Kuchukua Tahadhari ya Corona

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, amewataka watanzania kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Korona kama zinaelekezwa na wataalamu wa afya na amefafanua kuwa serikali haijazuia matumizi ya barakoa bali watanzania wachukue tahadhari kwa kutumia barakoa zinazotengenezwa hapa nchini.

 

Ameyasema hayo leo Februari 21 aliposhiriki kwenye misa takatifu  ya jumapili katika parokia ya mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam.

 

Rais Magufuli amesisitiza kutumia njia za asili za kukabiliana na magonjwa ya kupumua ikiwemo ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kujifukiza (kupiga nyugu)

 

Aidha Rais Magufuli amewataka watanzania kuondoa hofu inayopandikizwa ambayo ina madhara zaidi na amesisitiza kumtanguliza mungu mbele.

 

Amesema Wakristo ambao wapo katika kipindi cha Kwaresma na Waislamu ambao wanakaribia kuingia katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, waendelee kumuomba Mungu kwani pamoja na jitihada za kibinadamu kukabiliana na ugonjwa huo Mungu ndiye muweza wa yote na husimama kwa kila jambo.

 

Leave A Reply