The House of Favourite Newspapers

Wazee wa Baraza: Lulu Alimuua Kanumba Bila Kukusudia

0
Lulu mwenye (kilemba chekundu) akiwa amejiinamia, kulia ni mama yake na kushoto baba yake wakisubiri kesi kuanza.
Mama Lulu (kulia) akisubiri kwa umakini kesi ianze.
Ndugu wa Kanumba ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa mahakamani hapo.
Lulu akiondoka mahakamani huku amejifunika kanga baada ya kesi yake kuahirishwa.
…Akitolewa nje.
Mama Lulu akiingia kwenye gari ili kuondoka.
Mzee Michael Kimemeta akijiandaa kuingia kwenye gari.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ianze kusikiliza mfululizo kesi inayomkabili muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, wazee wa Baraza la mahakama hiyo leo wametoa maoni yake kuwa Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.
Katika maoni hayo yaliyotolewa na Jopo la Wazee watatu wa mahakama kwa nyakati fofauti, wote wamesema Lulu alimuua msanii mwenzake huyo bila kukusudia.
Awali kabla ya kutoa maoni yao, Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Sam Rumanyika,  aliwakumbusha wazee hao na mahakama kwa ujumla kuhusu maoni mbalimbali ya ushahidi wa pande zote mbili (utetezi na mashtaka) ambao tayari umeshawasilishwa na kusikilizwa mahakamani hapo.
Hatua hiyo ya wazee kutoa maoni yao imekuja  baada yakusikilizwa kwa ushahidi upande wa Jamhuri na upande wa utetezi ambapo jana yalisomwa mahakamani hapo maelezo ya mke wa Dkt. Slaa, Josephine Mshumbusi,  aliyekuwa daktari wa marehemu Kanumba enzi za uhai wake.

Muigizaji, Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa muigizaji wa filamu, Steven Kanumba bila kukusudia. Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7,2012, nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Jaji Rumanyika ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13 mwaka huu ambapo Mahakama hiyo itatoa hukumu.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

==

VIDEO: Lulu Alimuua Kanumba Bila Kukusudia – Wazee wa Baraza

Leave A Reply