The House of Favourite Newspapers

Waziri Aliyeripoti Kuibiwa Tsh. Bilioni 3 Nyumbani Kwake, Akamatwa

0
Cecilia Abena Dapaah

Cecilia Abena Dapaah aliamini anafanya uamuzi sahihi kwenda Polisi kuripoti lakini kibao kimegeuka na kushikiliwa kwa kumiliki kiasi kikubwa cha Fedha ambacho kinahusishwa na Rushwa

Inaelezwa ameibiwa Dola Milioni 1 (Tsh. Bilioni 2.4), Euro 300,000 (Tsh. Milioni 812) na Fedha ya Ghana cedis 350,000 (Tsh. Milioni 74), vingine ni begi la mkononi lenye thamani ya Dola 35,000 (Tsh. Milioni 85) na Vito vyenye thamani ya Dola 95,000(Tsh. Milioni 232)
Mwanasiasa huyo alitangaza kuachia ngazi baada ya tukio hilo lakini amesababisha hasira kwa Wananchi wengi kwa kuwa Fedha ya Ghana imekuwa ikishuka thamani miezi ya hivi karibuni huku ikidaiwa kuna Watu wachache wanaoficha Fedha za kigeni.

Leave A Reply