The House of Favourite Newspapers

Waziri Kangi Lugola Anusurika Ajali Morogoro

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, leo Jumatano, Oktoba 31, 2018  amenusurika kupata ajali wilayani Gairo, Mkoani Morogoro dereva wa baada ya Basi la  anoria mali ya Kampuni ya Hekima za Mungu kum-overtake kwenywe kona wakati gari la waziri huyo likiwa eneo sahihi.

 

Imeelezwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 6:04 mchana wakati Waziri huyo alipokua akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam, katika eneo la nje kidogo ya Mji wa Gairo.

Imedaiwa basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ lilikuwa na mwendokasi mkali wakati liki-overtake katika kona, ndipo dereva wa gari la Waziri Lugola alipunguza spidi ili kuiepuka ajali hiyo.

Aidha, basi hilo lilipopita, Waziri huyo aliekeza gari hilo lifuatwe kwa nyuma mpaka walikamate, hata hivyo basi hilo lilikamatwa na dereva wa basi hilo kukaguliwa kama alikua na sifa ya kua dereva.

 

Lugola alizungumza na abiria wa basi hilo ambalo lilikua linatoka Dar es Salaam kuelekea Mjini Kahama mkoani Shinyanga.

“Kwanini mnashindwa kukemea hii tabia ya huyu dereva, mnataka awaue?, alitaka kusababisha ajali mbaya sana hapa, nanyi mmekaa kimya, mnafanya makosa kutokuripoti hii tabia mbaya kabisa,” alisema Lugola.

 

Licha ya Dereva wa Basi hilo, Isaac Vian alikiri kosa hilo na kuomba msamaha lakini Waziri Lugola aliekeza akamatwe lakini atakapofika mwisho wa safari.

UPDATE : Zitto Akosa Dhamana, Asota Rumande

Comments are closed.