The House of Favourite Newspapers

Waziri Masauni: Hakuna Sababu ya Viongozi wa CHADEMA Kutorejea Nchini

0
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haioni sababu ya wanasiasa na viongozi wa CHADEMA kutorejea nchini.

 

Waziri Masauni ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali kuhusu mustakabali na hatima ya wanasiasa wa vyama vya upinzani walio nje ya nchi.

Waziri Masauni amesema watanzania wote hapa ni nyumbani kwao

Akiongea Bungeni Masauni amesema:

“Hakuna sababu yoyote kwa Mtanzania yoyote yule aliyepo sehemu yoyote ile ikiwemo viongozi hao wa Chadema kutorejea nchini, ili siyo tu waweze kutumia fursa nyingi ambazo nimezieleza za maendeleo hayo makubwa kiuchumi, kiusalama na kisiasa yaliyopo lakini kushiriki kikamilifu katika kutoa michango yao kwa maendeleo ya nchi yao katika nyanja zote kwani hapa ni nyumbani kwao.”

 

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lisu pamoja na viongozi wengine na wanasiasa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kama vile Godbless Lema wamekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu huku chanzo kikubwa kikihusisha migogoro ya kisiasa.

Leave A Reply