The House of Favourite Newspapers

Salim: Rais Samia Amezidi Kuifanya Tanzania Kuwa Kivutio Kikubwa cha Uwekezaji

0
Salim Aziz akiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya Dubai Expo.

 

Mfanyabiashara maafuru nchini Tanzania ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Bidhaa za Chakula wa Kampuni ya Bakhresa, Salim Aziz amesifu juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha mazingira bora ya uwekezaji nchini kutoka kwa wazawa na wageni.

 

Salim ambaye ni miongoni mwa Watanzania waliotajwa hivi karibuni na Jarida la Forbes Africa kuchangia kukua kwa uchumi wa Tanzania, amenukuliwa na jarida hilo akisema:

 

“Mheshimiwa rais ameleta ahueni kubwa ya kiuchumi kwa kipindi kifupi tangu alipoingia madarakani. Tanzania imeendelea kupokea wawekezaji wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani kutokana na kazi anayoifanya.

 

Salim Aziz

“Tanzania imerejea kwenye ramani na kuwa miongoni mwa nchi zinazovutia zaidi kiuwekezaji barani Afrika. Mwaka uliopita tumepokea wawekezaji wengi wa kigeni na wengine wengi wameonesha nia ya kuja kuwekeza. Kama hiyo haitoshi, tumekuwa tukisafirisha bidhaa nyingi kwenda nje ukilinganisha na majirani zetu.

 

“Mheshimiwa rais akiendelea na juhudi hizi, ndani ya muda mfupi ujao tutasimama imara kiuchumi kuliko wakati mwingine wowote na tutaweza kujitegemea kama taifa kwa sababu tunao utajiri wa kutosha wa rasilimali na utamaduni rafiki.

 

Wengine waliotajwa na Jarida la Forbes Africa kuchangia kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, ni Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Mohammed Dewji ‘Mo’ na wengine wengi.

Leave A Reply