The House of Favourite Newspapers

Waziri Mhagama Aongoza Maadhimisho Ya Kitaifa Ya Watu Wenye Ulemavu

mhagama1-1Waziri Jenista Mhagama akisoma hotuba yake katika maadhimisho hayo.

mhagama1-2Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Hamis akizungumza jambo.

mhagama1-3…Mhagama (kulia) akiimba na mtoto mlemavu (katikati) aliyekuwa akiimba wimbo wake.Pembeni wanayemuunga mkono ni viongozi waliokuwa kwenye hafla hiyo.

mhagama1-4Mmoja wa wananchi aliyefika kwenye maadhimisho hayo akimpa zawadi mtoto mlemavu wakati akiimba wimbo wake wenye hamasa kwa watu wenye ulemavu.

mhagama1-5Afisa Tawala wa Manispaa ya Ilala, Edward Mpogolo naye akizungumza jambo.

mhagama1-6Baadhi ya watu wenye ulemavu waliohudhuria maadhimisho hayo.

mhagama1-7Maadhimisho yakiendelea.

mhagama1-8Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule maalum za walemavu nao wakiwa katika maadhimisho hayo.

mhagama1-9Kikundi cha burudani kikisherehesha kwenye hafla hiyo.

Na Denis Mtima/GPL.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira naWalemavu, Jenista Mhagama leo ameongoza maadhimisho ya kitaifa ya siku ya watu wenye ulemavu jijini Dar.

Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar ambapo mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu ya ‘Ufanikishaji wa Malengo Endelevu 17 kwa Hatima Tuitakayo’.

Akizungumza katika hafla hiyo,Waziri Mhagama alilipongeza Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao stahiki.

Amesema taasisi au mashirika ambayo yalianzishwa kwa lengo la kusaidia watu wenye ulemavu lakini yanafanya kazi kwa manufaa binafsi anayaomba mara moja kuacha na akatoa rai kuwa hatasita kuyafutia usajili muda wowote.
Pia amevitaka baadhi ya vyombo vya habari kuhakikisha wakati wa matangazo yake vinakuwa na mkalimani wa lugha ya alama ili kuwawezesha wasiosikia kupata habari zinazotokea hapa nchini.

Comments are closed.