The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Aongoza Maelfu Kuaga Miili ya Waliofariki kwa Tetemeko Kagera

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa jana ameongoza maelfu ya waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera juzi Jumamosi.

Zoezi hilo lilifanyika katika Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na kidini.

Katika tetemeko hilo, watu 16 wameripotiwa kupoteza maisha huku 253 wakijeruhiwa, majengo 840 yakibomoka huku majengo 1264 yakipata nyufa.

Zifuatazo ni picha za tukio hilo;

tetemeko-5

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kuongoza zoezi la kuaga miili ya watu waliofariki kwa tetemo la ardhi.

tetemeko-6

Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare akitoa hotuba yake wakati wa zoezi hilo.

waziri-mkuu-bukoba

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima zake kwa miili ya watu waliopoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kulia kwake ni Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.

tetemeko-1 tetemeko-2 tetemeko-3 tetemeko-4

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasili katika Uwanja wa Kaitaba kuongoza zoezi la kuaga miili.

Comments are closed.