The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Awasilisha Taarifa Kuhusu Kimbunga Hidaya Bungeni – Video

0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa bungeni leo Mei 9, 2024 amewasilisha taarifa kuhusu kimbunga Hidaya.

Waziri Mkuu amesema kimbunga hicho kiliathiri nyumba zipatazo 2098 huku nyumba zaidi ya 600 kati ya hizo zikibomoka kabisa na nyingine zaidi ya 500 zikizingirwa na maji.

Mvua kubwa na upepo mkali zilizosababishwa na Kimbunga Hidaya zimesababisha vifo vya watu watano, kujeruhi wengine saba huku kaya zaidi ya 7000 zenye watu zaidi ya 18,000 zikiathirika.

Leave A Reply