The House of Favourite Newspapers

WAZIRI MKUU AZINDUA JUKWAA LA FURSA ZA BIASHARA TABORA – VIDEO

Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Novemba 21, 2018.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda ameupongeza mkoa wa Tabora kwa kuaandaa jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Saidi Kanimba  kuhusu viatu vya ngozi vinavyotengenezwa   katika Halmashuri ya wilaya Uyui mkoani Tabora katika Maonyesho ya  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yailyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. 

Amesema mkoa huo umefanya jambo zuri la kuandaa jukwaa hilo ambalo matunda yake yataunufaisha mkoa na taifa kwa ujumla.
Waziri Kakunda amesema kwa kujua umuhimu wa jukwaa hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye atakayelizindua.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sabuni za Kampuni ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora, Imani Matabula  (kulia)  katika  maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imani Matabula. 

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Tabora amempongeza Kakunda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Imani Matabula  (kulia)  kuhusu sabuni zinazotengenezwa na Kampuni yake ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora katika maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Amesema hiyo inadhihirisha imani kubwa aliyonayo Rais John Magufuli kwake na wananchi wa Tabora.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwinga amewahakikishia usalama na mazingira mazuri ya biashara wawekezaji wanaotaka kwenda kuwekeza kwenye wilaya hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa yenye ujazo wa nusu lita ya mkojo wa sungura wakati alipotembelea banda la wanamama  wajasiriamali wasindikaji wa Tabora. Kwa mujibu wa Mratibu wa Wajasiriamali hao, Bibi Ashura Mwazembe, mkojo wa Sungura unatumiwa kama mbolea ya mazao ya kilimo na pia ni dawa nzuri sana ya kuua wadudu waharibifu wa mazao. Lita moja ya mkojo huo inauzwa sh. 10, 000/=. 

Amesema wilaya yake inafaa kwa uwekezaji kwa kuwa ina barabara nzuri na ina maeneo ya kutosha kwa ajili ya kilimo na viwanda.
Pia alisema wilaya hiyo imebarikiwa kuwa na vitalu vya utalii na mazao ya misiti ikiwamo asali inayosifika kwa ubora nchini.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimina na Kaimu Mhariri Mtendaji wa  Magazeti ya Serikali (TSN),  Tuma Abdallah (kushoto) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege  wa Tabora kushiriki katika  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora, Novemba 21, 2018.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

RC Mwanri Amvunja Mbavu Waziri Mkuu “Nchi inakata roho”

 

Comments are closed.