The House of Favourite Newspapers

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUTIKISA LINDI LEO

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kuwasili mkoani Lindi leo Mei 21, 2018 ambapo atazindua mradi wa kuunganisha mkoa huo na wa Mtwara katika gridi ya Taifa.

 

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa jana Mei 20 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Waziri Mkuu ambapo alieleza Majaliwa atazindua miradi mikubwa mitatu ukiwamo wa kuunganisha Lindi na Mtwara kwenye gridi ya taifa.

 

Pia, Waziri Majaliwa atakagua miundombinu ya uingizaji mafuta katika mkoa huo ambao unatarajia kuanza kupokea mafuta ya petroli na dizeli mwezi ujao.

 

“Atakwenda kujionea miundombinu ya uingizaji mafuta kupitia bandari ya Mtwara, habari njema iliyopo kuanzia Juni utaanza kupokea mafuta kupitia bandari ya Mtwara,” alisema Byakanwa.
Alisema Waziri Mkuu atakwenda kwenye uzinduzi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme Mtwara ambapo miundombinu ya Bandari ya Mtwara itakuwa na uwezo wa kupokea lita 25 milioni za mafuta lakini kwa kuanzia Juni wataanza na lita 10 milioni.

“Kampuni mbili tayari zimeshaagiza mafuta lita 10 milioni, wafanyabiashara wengine sasa waone Mtwara kama sehemu ya fursa na itapunguza msongamano,” alisema.

Comments are closed.