WAZIRI MKUU MGENI RASMI SIMBA DAY UWANJA WA TAIFA LEO

SIMBA leo wanafika kilele cha SportPesa Simba Wiki ambapo uwanja wa Taifa kutachezwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Power Dynamo.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema:”Tunajua kwamba wenzetu wamefanya kitu kizuri ila sisi ni hatua nyingine hasa kwa ubunifu na ubora wa kile ambacho tunakifanya mwanzo mwisho.

“Kila kitu kipo kwenye mpangilio bora na staili ambazo zitatumika kwenye utambulisho wa wachezaji haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa nchi.

“Hapa ni chuo cha ubunifu hivyo nawaambia mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa kushuhudia namna tutakavyofanya,” amesema.

 


Loading...

Toa comment