The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Dereva wa RC Aliyepata Ajali Afariki Dunia

MTOTO wa dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kasobi Shida ( 26), aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Kaimu Mganga Mfawidhi, Dkt.  Hosea Bisanda amethibitisha.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo amesema kimetokea kwa sababu ajali aliyoipata ilikuwa ni mbaya,  hali iliyopelekea kijana huyo kupata majeraha mwilini.

 

”Ni kweli amefariki na sababu ya kifo chake, baada ya madaktari kumfanyia upasuaji,  waligundua utumbo wake ulikuwa umepasuka na damu ilivujia ndani kwa ndani, ‘ amesema RPC Ndaki.

 

Akielezea hali ya dereva wa Mkuu wa Mkoa (baba wa marehemu), amesema hali yake inaendelea vizuri na kwamba madaktari wanaendelea kumfanyia ushauri wa kisaikolojia ili arejee kwenye hali yake ya kawaida.

 

Kasobi alipata ajali siku ya Agosti 4, 2019,  baada ya kuchukua gari hilo bila ridhaa ya mzazi wake ambapo lilimshinda kuendesha na kutoka nje ya barabara kisha kugonga daraja.

 

 

 

 

 

Comments are closed.