The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu wa Italia Atangaza Kujiuzuru, Ugumu wa Maisha Watajwa kama Sababu

0
Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi

WAZIRI Mkuu wa Italia Mario Draghi amethibitisha kutuma barua kwa rais wa nchi hiyo Sergio Mattarella kutaka kujiuzuru wadhifa wake kutokana na kuwepo hali ya kutoungwa mkono na wafuasi wa chama chake.

 

Kujiuzuru kwa Waziri Mkuu huyo kunafungua milango ya uchaguzi mkuu mapema mwezi Septemba au Oktoba mwaka huu, huku taaifa kutoka Ikulu ya Italia ikibainisha kuwa Rais Mattarella bado hajaweka bayana kuhusu taratibu za kulivunja Bunge hilo.

 

Draghi ambaye ambaye alikuwa Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya aliingia madarakani mwaka 2021 wakati Italia ikipambana na maambukizi ya Uviko-19.

Waziri Mkuu Mario Draghi ameshutumiwa kwa kosa la kushindwa kutatua changamoto ya kupanda kwa gharama za maisha

Ripoti imebainisha kuwa Draghi alipanga kujiuzuru tangu wiki iliyopita kufuatia moja ya wafuasi wa chama chake kushindwa kumuuunga mkono katika kura za kuwa na Imani naye huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kupanda kwa gharama za maisha katika nchi hiyo.

 

Kwa upande mwingine imebainika kuwa Rais Mattarella alikataa ombi la kujiuzuru kwa Waziri Mkuu huyo na kumuagiza arudi Bungeni na kutafuta suluhu ya namna ya kuwaunganisha wabunge pamoja na kutatua changamoto hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2023.

Leave A Reply