The House of Favourite Newspapers

Manara Afungiwa Kujihusisha na Soka kwa Miaka 2, Apigwa Faini ya Milioni 20.

0
Kamati ya Maadili imemfungia Msemaji wa Yanga Haji Manara kutojihusisha na soka kwa kipindi cha mika 2 na faini ya Milioni 20 za kitanzania

KAMATI ya Maadili ya TFF imetoa hukumu ya kumfungia Msemaji wa Yanga Haji Manara kujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka miwili (2) pamoja na faini ya shilingi milioni 20.

 

Kamati imetoa hukumu hiyo leo Julai 21, 2022 ikiongea na waandishi wa habari ambapo imesema imemkuta Manara na kosa la kumtukana Rais wa TFF Wallace Karia.

 

Kamati imebainisha kuwa Manara alikutwa na hatia kutokana na kutoa baadhi ya matamshi ambayo yaliashiria kumdharirisha Rais wa TFF.

Msemaji wa Yanga Haji Manara

Shauri hilo namba 2 la kesi ya maadili lilifunguliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF dhidi ya Msemaji wa Yanga Haji Manara na Kamati ya maadili ya TFF ikakutana kwa mara ya kwanza Julai 11, 2022 kusikiliza shauri hilo.

 

Aidha kamati hiyo imebainisha kuwa adhabu hiyo inaanza leo Julai 21, 2022 na Manara anayo haki ya kukata rufaa juu ya uamuzi huo.

Leave A Reply