The House of Favourite Newspapers

Waziri Ummy: Wazembe Watupishe

0

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Ummy Mwalimu, amesema atazifumua Sekretariet za Mikoa endapo hazitatekeleza majukumu yake ipasavyo.

 

Waziri Ummy ameyasema katika kikao cha Sekretariet ya Mkoa wa Tanga iliyoketi katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

 

Amesema “Jicho langu la karibu ni Sekretarieti za Mikoa sitaki nianze kupambana na Halmashauri 184 wakati nina watu kwenye Sekretarieti za Mikoa ambao wako karibu kimazingira na kiutendaji na halmashauri hizo ninataka watekeleze majukumu yao ipasavyo na mimi nipate taarifa zote kutoka kwao.

 

Amesema endapo Sekretarieti ya mkoa ambayo atabaini wataalam wake ni wazembe na hawatekelezi majukumu yao ipasavyo itabidi wapishe.

Leave A Reply