Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Angellah Kairuki Akabidhi Mizinga 200 Kwa Wafugaji
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki, Novemba 20, 2021 amekabidhi mizinga takribani 200 kwa wafugaji wa nyuki wa Gairo, Morogoro, ikiwa ni sehemu ya mizinga zaidi ya 500 itakayotolewa pia katika wilaya nyingine nchini ikiwa ni mchango wa Benki ya NMB kuunga mkono juhudi za Serikali kukuza sekta ndogo ya Misitu na Nyuki nchini.
Huu ni wajibu wa kimkakati kwa jamii chini ya NMB na tunawakaribisha wadau wengine katika sekta hii inayotoa ajira takribani milioni 2 kwa sasa na kuchangia kwa asilimia 3.5 katika Pato Ghafi la Taifa (GDP).