The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba Akutana na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya

0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (kulia) akiwa na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. Musalia Mudavadi walipokutana jijini Kampala

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba amekutana na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. Musalia Mudavadi walipokutana jijini Kampala, Uganda pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) tarehe 17 Januari 2024.

Mawaziri hao walijadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Mataifa yao na kuahidi kuendelea kutumia majukwaa ya kidiplomasia kutatua changamoto zinazokwamisha ustawi mzuri wa Biashara, uwekezaji, utalii na uendelezaji wa miundombinu kwa manufaa ya pande zote mbili.

Leave A Reply