The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Uingereza Masuala ya Afrika, LATAM na Visiwa vya Caribbean Atembelea Serengeti

0
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Latini Amerika na Caribbean Mhe Vicky Ford (wa pili kutoka kushoto) akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha SBL kilichopo Moshi katika ziara yake mkoani Kilimanjaro ambapo alijionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na SBL ambayo inamilikiwa na kampuni mama ya Uingereza, Diageo.

 

 

MOSHI, Tanzania; Aprili 3, 2022: Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Latini Amerika na Caribbean Vicky Ford, leo ametembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Latini Amerika na Caribbean Mhe Vicky Ford (wa pili kulia) akionyeshwa maeneo mbalimbali kiwandani hapo na Felix Alala, Meneja Miradi wa SBL (wa kwanza kulia).

 

 

Katika ziara yake alifanya mazungumzo na uongozi wa SBL na kukutana na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na SBL ambayo inamilikiwa na kampuni mama ya Uingereza, Diageo.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Latini Amerika na Caribbean Mhe Vicky Ford akionyeshwa uzalishaji wa pombe kali unavyofanyika kinachosimamiwa na wafanyakazi wanawake pekee.

 

 

SBL ni kampuni kubwa inayozalisha bia na pombe kali, pia ni moja kati ya walipa kodi wakubwa na mchangiaji mkubwa wa uchumi wa nchi. SBL inaendesha programu nyingi za kuisaidia jamii ikiwa ni pamoja na miradi ya maji, upandaji miti, wakulima wazawa wanaolima mazao yanayotumika katika uzalishaji wa bia zake kama shayiri, mahindi na mtama. Asilimia 80 ya malighafi inazotumia SBL kuzalisha bia, inazipata kutoka wakulima wa ndani.

 

“Nimefurahishwa kuona ujumuisha mkubwa wa wanawake katika shughuli za Kampuni ya Bia ya Serengeti na pia progamu zake za kusaidi jamii ya kitanzania,” alisema Ford, muda mfupi baada ya ziara yake katika kiwanda cha pombe kali cha Moshi kilichozinduliwa mwaka jana kinachoendeshwa na wafanyakazi wanawake tu,”.

Leave A Reply