The House of Favourite Newspapers

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI WA LESOTHO ATEMBELEA MRADI WA DART

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (aliyesimama) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho walipotembelea mradi huo.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bw. Hija Malamla akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wataalamu wa sekta ya barabara nchini na ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho uliko nchini kwa ziara ya mafunzo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele (wa pili kulia) akisisitiza jambo kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya ujumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bw. Lyanga (wa pili kushoto) akiwasilisha mada kwa ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho walipotembelea ofisi za TANROADS jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Moramotse (kulia) alipotembelea kukagua mradi huo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (wa tatu kulia) akisisitiza jambo akiwa kwenye moja ya Mabasi yaendayo haraka (DART) alipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare.

Comments are closed.