The House of Favourite Newspapers

Wazungu wamfuata Samatta Dar

0

Ibrahim Mussa na Martha Mboma
WAKATI timu tatu kutoka nchi za Ufaransa na Ubelgiji zikiweka ofa mezani kwa ajili ya kumpata straika wa TP Mazembe, Mtanzania, Mbwana Samatta, meneja wake, Jamal Kisongo, amefunguka kuwa tayari wameshamalizana na viongozi wa timu mojawapo ambao walitua Dar hivi karibuni.

Samatta amekuwa akiwindwa na klabu tofauti za Ulaya kutokana na kiwango chake kwa sasa, lakini akitoa masharti likiwemo la kutofanya majaribio kwa timu ambayo inamhitaji.

Hii ni baada ya kumaliza majukumu yake ya klabu yake ya TP Mazembe katika ile michuano ya Klabu Bingwa Dunia hivi karibuni.

Kisongo amesema: ”Naweza kusema Samatta tayari amepata klabu ila kwa sababu dirisha la Ulaya halijafunguliwa, ndiyo tunashindwa kusema ni timu ipi imemchukua kwa sababu viongozi wa klabu yake pamoja na Wazungu walikuja hapa nchini hivi karibuni tukaongea na kuweza kuipitisha mikataba yote.”

“Inakuwa ngumu kutangaza kuwa amechukuliwa na timu ipi mpaka sasa, wapenzi wa soka wawe wavumilivu mpaka Januari ndipo tunaweza kuanika kila kitu.

“Na hili tulipanga kulikamilisha mara baada ya michuano ile ya Klabu Bingwa Dunia, tuliamini Mazembe ingefanya vyema lakini mambo yalikwenda tofauti,” alisema Kisongo.

Leave A Reply