The House of Favourite Newspapers

WEMA APANGUA RATIBA TAMASHA LA TWANGA PEPETA

Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Chalz Baba,  akifanya yake kwenye Ukumbi wa The Legends, 

TAMASHA la kihistoria la kuadhimisha miaka 20 ya Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, lililopangwa kufanyika Septemba 29, mwaka huu, limesogezwa mbele kwa sababu zisizoweza kuzuilika. Akizungumza na Global Publishers, Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, alisema wameamua kulisogeza mbele tamasha hilo hadi Oktoba 06, mwaka huu lakini pia wamebadilisha ukumbi wa kufanyia tamasha hilo.

Alisema, badala ya kufanyika The Legends Club, sasa litafanyikia katika ukumbi wa The Life uliopo Mwenge.

“Tumebadilisha siku ya kufanya tamasha kwa sababu ya kupisha matukio ambayo yatakuwa yanafanyika siku za karibuni za tamasha hilo.

“Kwanza tumeamua kumpisha Wema na sherehe yake ya kuzaliwa ambayo itafanyika Septemba 28, na mechi ya watani wa jadi, tunafahamu wapenzi wa muziki wetu ndiyo mashabiki wa Wema, ndiyo wapenzi wa mpira pia, kuliko kuwarundikia burudani wakati mmoja bora sisi tusogee mbele na kuwapa nafasi kuhudhuria ‘events’ hizo nyingine,” alisema Asha Baraka.

Asha aliongeza kwamba sababu za kubadilisha ukumbi ni kupeleka tamasha hilo kwenye ukumbi mkubwa zaidi kutokana na mwamko kuwa mkubwa na kuonekana pale The Legends Club hapatatosha.     

Matukio katika Picha

Mama wa mwanamuziki Kalala Junior (kushoto) akishuhudia onesho la Twanga Pepeta  jana.
Wadau wa Twanga Pepeta wakiwa kwenye pozi wakati wa onyesho la bendi hiyo.

Chalz Baba akioga pesa kutoka kwa shabiki wa Twanga aliyekunwa na onyesho la bendi hiyo.

Densa wa Twanga akimwaga radhi kwa mauno.

Mkurugenzi wa Twanga, Asha Baraka (kushoto) akimsapoti mdau wa muda mrefu wa Twanga aliyekuwa anakata keki katika onesho hilo la jana ikiwa ni ishara ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Stori: Boniphace Ngumije 

 

Comments are closed.