The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Apiga ‘STOP’ Kucha na Kope Bandia Bungeni – Video

Spika wa Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai leo Septemba 10, 2018 amepiga marufuku wabunge wanawake kuingia Bungeni wakiwa wamebandika kucha na kope za bandia huku akiendelea kuchukua maoni ya nini kifanyike kwa waliojichubua.

Marufuku hiyo imetolewa baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Taufiq kuuliza swali la nyongeza kuhusu madhara ya vipodozi hivyo huku akiitaka serikali kuchukua hatua.

“Kwa vile swali hili ni muhimu sana na Waziri amesema sisi wabunge tuwe mfano, kwa mamlaka mliyonipa, napiga marufuku kabisa kwa wabunge kuingia humu wakiwa na kucha na kope za kubandika, lakini kwa waliojichubuka (mkorohgo) bado naendelea kuchukua maoni,” amesema Ndugai.

VIDEO: SHUHUDIA MAAMUZI YA NDUGAI

Comments are closed.