The House of Favourite Newspapers

WEMA APOKELEWA KWA SHANGWE NA WAHARIRI GLOBAL (PICHA + VIDEO)

Mwigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu akisani kitabu cha wageni katika ofisi ya Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam leo.

 

MWIGIZAJI maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu, leo Ijumaa, Julai 26, 2019,  amepokelewa kwa shangwe na wahariri wa Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Championi na Spoti Xtra, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam alipokuja kutambulisha ujio wake mpya wa ‘Wema Empire’ ambao utahusika na uandaaji wa filamu nchini.

…Akiwa na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers,  Saleh Ally.

Mrembo huyo amesema Julai 27, 2019,  itakuwa siku atakayofanya usaili (audition) wa kusaka vipaji vya waigizaji  utakaofanyika katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambao wakakaofaulu, utawawezesha kupata fursa ya kushiriki  kwenye tamthilia mbalimbali ambazo zitaandaliwa chini ya himaya yake.

Usaili huo utakaofanyika saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni utahusu wanaume wenye kuanzia miaka 26 hadi 35, wanawake miaka 22-30, kinababa miaka 45-60 na kinamama miaka 45-60.

…Akikabidhiwa Gazeti la Amani na mhariri wake, Erick Everest.
…Akikabidhiwa  Gazeti la Risasi Mchanganyiko na mhariri wake, Andrew Carlos. 
…Akikabidhiwa Gazeti la Uwazi, na Mhariri Amrani Kaima.
…Akikabidhiwa Gazeti la Championi Jumamosi na Mhariri Lucy Mgina. 
…Akikabidhiwa Gazeti la Betika na Mhariri  Msaidizi Omary Mdose.
…Akikabidhiwa gazeti la Spoti Xtra na Martha Mboma.

 

Comments are closed.