The House of Favourite Newspapers

WEMA JELA MIAKA SABA, TCRA WAMKALIA KOONI

SOO lake la picha na video za ngono mtandaoni linazidi kumkalia vibaya staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Ijumaa Wikienda limedokezwa.

Kwa kesi aliyofunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita, endapo itathibitika kwamba kweli ana hatia, adhabu yake ni kifungo cha miaka saba (7) jela au faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja.

 

Mbali na kufungiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kujihusisha na masuala ya filamu kwa muda usiojulikana, pia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imemkalia kooni baada ya kumfungulia kesi ambayo sasa itamlazimu kupanda kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.

 

Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi, Wema alifunguliwa shitaka hilo Ijumaa iliyopita kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kituoni hapo na Ofisa wa Teknolojia ya Mawasiliano ya Intaneti wa TCRA aliyetajwa kwa jina la Frank Bizuru, Wema anashitakiwa kwa kosa la kuchapisha na kusambaza maudhui ya kingono mtandaoni.

 

Shitaka hilo lilifunguliwa jalada la kesi namba KJN/ RB/13607/2018-KUCHAPISHA NA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO MTANDAONI.

Taarifa hiyo ya kipolisi ilieleza kuwa, TCRA walibaini kosa hilo Oktoba 25, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi kwenye ofisi za mamlaka hiyo kuwa mtuhumiwa alisambaza picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

 

Ilielezwa kwamba, mara baada ya kukamatwa kwa Wema ambaye alikuwa anatafutwa na Polisi mwishoni mwa wiki iliyopita, atafikishwa mahakamani mara moja.

Ilidaiwa kwamba, kesi hiyo itakapofika mahakamani, endapo Wema atathibitika kufanya kosa hilo atakabiliana na adhabu ya hukumu hiyo.

 

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, endapo mtuhumiwa atabainika kusambaza picha au video za ngono au zinazoashiria vitendo vya ngono, adhabu ya kosa hilo ni pamoja na faini ya shilingi milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka saba jela au vyote kwa pamoja.

 

Kwa mantiki hiyo, kama Wema atakutwa na hatia katika shitaka hilo atakumbana na adhabu ya faini ya shilingi milioni 20 au kwenda jela miaka saba au vyote kwa pamoja.

Hivi karibuni Wema alidaiwa kusambaza picha zenye maudhui ya kingono kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Patrick Christopher ‘PCK’ na kuibua gumzo kubwa.

STORI: Sifael Paul, DAR

LIVE: KUAGWA KWA ISACK GAMBA, MAJONZI & VILIO VYATAWALA

Comments are closed.