The House of Favourite Newspapers

Nyoni, Juuko Wampa Wakati Mgumu Mbelgiji

BAADA ya hivi karibuni Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems kufanikiwa kuiona pacha ya mabeki wake wawili wa kati, Mganda, Juuko Murshid pamoja na Pascal Wawa, raia wa Ivory Coast, sasa ameanza mchakato wa kutaka kuiona pacha nyingine ya Juuko na Erasto Nyoni.

 

Aussems anataka kuiona pacha hiyo ili aweze kuamua ni pacha gani ambayo inastahili kuwa katika kikosi chake cha kwanza kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Bara lakini pia ile ya kimataifa ambayo timu hiyo itashiriki mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Aussems alisema kuwa kabla ya kumuona Juuko uwanjani, alikuwa akijivunia pacha ya Wawa na Nyoni.

 

Lakini baada ya kumuona Juuko akicheza kwa kiwango cha juu akishirikiana vyema na Wawa, alivutiwa pia na pacha hiyo na kujikuta akitamani kui­ona pacha ya Juuko na Nyoni.

“Nimeijaribu pacha hiyo mazoezini na nimeona jinsi inavyocheza kizuri lakini na­taka nione pia katika mechi.

 

“Kwa hiyo, Nyoni akimaliza adhabu yake ipo siku nita­waanzisha pamoja na Juuko ili niweze kuwaona na baada ya hapo sasa ndipo nitaka­pojua ni pacha gani ambayo inastahili kuwa katika kikosi changu cha kwanza,” alisema Aussems.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

OKWI Alivyokabidhiwa Mpira Baada ya Kupiga Hat Trick

Comments are closed.