The House of Favourite Newspapers

Wema: Mama Whozu Amenikubali, Nimepitia Maisha ya Kusimangwa na Watu

0
Wema Isaac Sepetu au Tanzania Sweetheart akiwa na mpenzi wake Whozu.

Wema Isaac Sepetu au Tanzania Sweetheart; ni supastaa wa filamu nchini Tanzania ambaye kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kukubalika na mama mzazi wa mpenzi wake wa sasa ambaye Whozu.

 

Mara baada ya Wema kuthibitisha kuwa kwenye penzi zito na Whozu huku wakijiita Chimama na Chibaba, kuliibuka habari za mitandaoni kwamba familia ya Whozu akiwemo mama yake hawataki kabisa kusikia habari za mtoto wao kutoka kimapenzi na mlimbwende huyo.

Msanii Whozu.

Habari hizo zilidai kuwa, familia hiyo inamkubali mno video vixen Tunda ambaye amezaa na Whozu huku wakimuona Wema ni mkubwa kwa Whozu.

 

Hata hivyo, kupitia kipindi chake cha My Truth kinachrushwa kwenye Wemaapp, staa huyo anasema kuwa, mama Whozu anampenda na kumkubali kama ambavyo na yeye anampenda na kumkubali.

 

“Kitu kimoja ambacho naweza kukisema ni kwamba mama mkwe ninampenda na ananipenda hivyo tu,” anasema Wema na kuongeza;

 

“Nimepitia maisha mengi sana, nimepitia maisha ya kusimangwa, ikafika muda nikaona kama nimekata tamaa, lakini kwa sasa hivi sina msongo wa mawazo, mbona kwa sasa hivi nipo sawa sana?

 

“Sihitaji msaada wa mtu yeyote tena nasema sihitaji msaada wa mtu yeyote, kwa sasa nipo sawa sawia,” anasema Wema ambaye penzi lake na Whozu limekolea mno.

STORI NA SIFAEL PAUL |  GPL

HUU HAPA UJIO MPYA WA SELINA NA TAMTHILIYA YA YALAITI KUPITIA DSTV MAISHA MAGIC EAST…

Leave A Reply