The House of Favourite Newspapers

WEMA: NINA KITU WENGINE HAWANA!

Wema Isaac Sepetu

BAADA ya kusemwa mengi kuhusiana na jina la Tanzania Sweetheart, mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hayupo tayari kuacha kulitumia kwani ana kitu ambacho wengine hawana na haoni mtu wa kumrithi.

Wema ameliambia Risasi Jumamosi kuwa, hawezi kustaafu kutumia jina hilo kwa sababu wakati anapewa na mashabiki wake wa jijini Arusha, hakuambiwa kama kuna kustaafu hivyo jina hilo ni lake na ataendelea kulitumia.

“Kwani kuna kustaafu? Sasa nani mwingine atumie jina hilo wakati Tanzania Sweetheart ni mmoja tu? Kwanza akianza kulitumia mtu mwingine mashabiki watakubali? Kila kitu kinaenda na mazoea, watu wamenizoea mimi na nitabaki kuwa mimi tu na hakuna kama mimi,” alisema alisema Wema akicheka. Hivi karibuni kumeibuka ushindani wa mashabiki juu ya nani alitumie jina hilo kati ya Wema na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

STORI: Shamuma Awadhi, Dar

Comments are closed.