The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Afunguka Mazito Akataa Aibu, Napenda Kuigiza, Kuimba Siwezi

0
Wema Isaac Sepetu

WEMA Isaac Sepetu; ni muigizaji mkubwa nchini Tanzania ambaye amesema kuwa hana mpango wa kujitosa kwenye muziki wa Bongo Fleva kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

 

Wema au Last Born wa Taifa anasema kuwa, ana uwezo wa kuingiza sauti yake kwenye nyimbo za wasanii, lakini siyo kusimama mwenye kama msanii wa muziki.

 

Anasema; “Mimi huwa napenda kuingiza zile sauti za nyuma, kuimba siwezi, sitaki kujitia aibu, kama wasanii wanapenda sauti zile za nyuma, mimi niko vizuri hamna wimbo wowote wa Wema unakuja.

 

“Sitegemei kuingia kwenye kuimba kwa kweli. Mtanicheka nikianza kuimba, siko tayari.”

Wema anasema kuwa, amewahi kuingiza sauti yake kwenye nyimbo kadhaa za aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz; nyimbo hizo ni ni Lala Salama na Chanda Chema.

 

Wema ametoa msimamo wake huo baada ya kuwepo kwa msururu wa mastaa wa kike wa Bongo Movies kukimbilia kwenye muziki kama alivyofanya Rose Ndauka, Lulu Diva na wengine.

Cc; @sifaelpaul

TANZANIA vs ALGERIA: HALI Ilivyo UWANJANI, MASHABIKI wa STARS WAFURIKA, AFE KIPA, AFE BEKI, POINT 3!

Leave A Reply