The House of Favourite Newspapers

Wema: Snura ndo Rafiki Yangu wa Milele Mpaka Naingia Kaburini Ninampenda – Video

0
Tanzania Sweetheart Wema Sepetu

 

WEMA SEPETU Mrembo mwenye nyota yake kunako tasnia ya Filamu na urembo nchini amesema kwamba msanii Snura Mushi ndiye rafiki yake wa milele na wa thamani aliyewahi kutokea katika maisha yake na kwamba ataendea kumpenda leo hadi siku atakapokufa.

Snura ni Mwanamuziki na Muigizaji wa Bongo Muvi

 

Wema ambaye ni mshindi wa taji la Miss Tanzania mwaka 2006 amesema hayo hivi karibuni wakati akihojiwa na wanahabari jijini Dar es Salaam.

 

Alipoulizwa kwa nini siyo marafiki zake wengine kama Lulu Diva, Kajala au Aunty Ezekiel ambao wameonekana kuwa karibu na yeye mara nyingi, Wema amesema Snura amekuwa akimshauri mambo mazuri na ya hekima na kuna wakati alikwama kwenye maisha lakini Snura alimsaidia msaada ambao hautafutika hadi leo.

 

Wema amesema kuna baadhi ya marafiki zake aliwasaidia lakini matokeo yake walikuja kumuumiza na kumsaliti, hivyo heshima kubwa itabaki kwa Snura kama rafiki wa kweli na namba moja kwa Wema.

Leave A Reply