The House of Favourite Newspapers

Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 30 kwa Kosa la Kumbaka Mwanafunzi

0
Faison Sanga ahukumiwa kifungo cha miaka 30 Gerezani kwa kosa la ubakaji

MAHAKAMA ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imemuhukumu Faison Sanga ( 19 ) mkazi wa Makwaranga Kata ya Ipelele kutumikia kifungo cha miaka 30 Gerezani kwa kosa la ubakaji.

 

Mnamo Februari 2, 2022 Bwana Faison Sanga anatajwa kufanya kitendo hicho cha ubakaji kwa mwanafunzi wa shule ya msingi ( 15 ) .

 

Kosa hilo la ubakaji ni kinyume na kifungu cha 130 ( 1 ) ( 2 ) e na 131 ( 1 ) ya kanuni ya adhabu sura ya 16 Marejeo 2019 .

Aidha Bwana Sanga ameiomba Mahakama kuweza kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana familia inayomtegemea.

 

Kwa upande wa mashtaka uliiomba Mahakama kuweza kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine ambao wamekuwa wakikatisha masomo ya watoto wa kike.

Mahakama ya Wilaya ya Makete

Kwa upande wa mashtaka mashahidi wa kesi hiyo walikuwa wanne ambao ni muhanga mwenyewe,baba wa mtoto,Daktari kutoka hospitali ya wilaya ya Makete pamoja na G3615 Dictective Coplo Benedicto .

 

Hukumu hiyo imetolewa hapo jana na hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Makete Mh.Ivan Msaki pamoja na Inspecta wa jeshi la polisi Benstard Mwoshe Wilaya ya Makete.

Leave A Reply