The House of Favourite Newspapers

WHO: Vifo Vitokanavyo na Virusi vya Corona Vyadizi Kupungua Duniani

0
                                                                       Virusi vya Covid- 19

SHIRIKA la Afya Duniani limerekodi idadi ndogo zaidi ya virusi vya Corona tangu machi 2020, mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hayo wakati akitoa mwenendo wa ugonjwa huo.

 

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema dunia haijawahi kuwa katika nafasi nzuri ya kukomesha COVID-19, kuliko wakati huu.

                            Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus

Katika ripoti yake ya kila wiki kuhusu janga hilo, shirika la afya la Umoja wa Mataifa lilisema vifo vilipungua kwa asilimia 22,  wiki iliyopita.

 

Hata hivyo, WHO ilionya kuwa kulegea kwa juhudi za upimaji na ufuatiliaji kunamaanisha kuwa visa vingi vya Covid 19 haviripotiwi.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply