Rais Samia Asikitishwa na Kifo cha Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bi Fatma Omar Latu pamoja na dereva wake kilichotokea jana Septemba 14, kwa ajali gari iliyotokea mkoani Mbeya.
Kupitia ukurasa wake rasmi kwenye mtandao wa Twitter Rais Samia ameandika “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bi. Fatma Omar Latu pamoja na dereva wake kilichotokea tarehe 14 Septemba kwa ajali ya gari mkoani Mbeya. Mungu azilaze roho zao mahala pema Peponi” Amin.
Ajali hiyo imehusisha pia magari mengine mawili, likiwemo lori la kubebea mafuta, mali ya kampuni ya Lake Oil na lori lingiine la mizigo.